Philippians 1:1-6

Salamu

1 aWaraka wa Paulo na Timotheo, watumishi wa Al-Masihi Isa:

Kwa watakatifu wote katika Al-Masihi Isa walioko Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi:

2 bNeema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe nanyi.

Shukrani Na Maombi

3 cNinamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. 4 dKatika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, 5 ekwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. 6 fNina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Al-Masihi Isa.

Copyright information for SwhKC